| Who | When |
Messages | |
|
|
|
ndesanjo
|
1
|
 |
|
05-21-2005 10:41 AM ET (US)
|
|
Mimi naanza kwa kusema kuwa nimekubalina kabisa na hoja ya msingi ya Tungaraza. Nadhani tumekuwa wavivu tukaamua kuchukua neno la kiingereza "blog" na kulilazimisha kuwa la Kiswahili.
Haya uwanja u wazi...
|
| ndesanjo
|
2
|
 |
|
07-15-2005 02:42 PM ET (US)
|
|
Nkya wa pambazuko.blogspot.com ametoa wazo kuwa blogu iitwe Bawazi. Namuomba atufafanulie kidogo msingi wa chaguo lake hili. Mimi kweli bado nafikiria.
|
| Nambiza Tungaraza
|
3
|
 |
|
07-17-2005 08:39 AM ET (US)
|
|
Hili suala lina utata. Nikisema blogu kazi yake ni kuandika mawazo au kumbukumbu kwa uwazi ni sawa. Ikesha iko kwenye mtandao, hivyo ni kifaa-pepe. Lakini kila nikitunga neno, linakuwa refu wala halivutii kusema, mfano:
Ki-faa, pe-pe, ma-wazo, kumbu-kumbu, tovuti. Basi nachanga-changa halafu napata neno kama:
-Tovuti-mawazo -Tovuti-kihifadhi-mawazo -Nk, NK, Haina shaka, tutafika
|
| Indya Nkya
|
4
|
 |
|
07-20-2005 01:23 PM ET (US)
|
|
Sababu ya kupendekeza neno BAWAZI ni kwamba ukweli ni kwamba teknolojia hii imetuwezesha kuwasiliana na kuweka mambo mengi wazi na hakuna vikwazo kabisa. Kwa hiyo WAZI nimefikiria kwa msingi huo. BA ni kiunganishi tuu. Mjadala uendelee
|
| Da Mija
|
5
|
 |
|
12-26-2005 12:19 PM ET (US)
|
|
Ninapendekeza neno NGWANGA, neno hili ni jipya na halina maana yoyote. Baada ya kupiga akili nikaona ni vyema nilitengenezee maana ili nitakapoulizwa nisishindwe cha kujibu. Tukiangalia maana ya blogu tunaona ni uandishi wa habari wa mtandaoni usiokuwa na mipaka, unaweza kuandika lolote lile katika chochote kile, hivyo nikachukua neno "GWA" kama tukio na neno "NGA" kama reaction ya mwandishi. Waswahili wakati mwingine huita kitu na box...Jambo likitokea tu ..GWAAA!!..Mwandishi naye palepale anapiga.. NGAAA!! kwa kuliweka hadharani.
Jamani tuendeleeni, mimi haya nimeyatunga kwa vile naamini hakuna lililoshushwa, yote tuliyoyakuta yalianzishwa namna hii.
|
| ndesanjo
|
6
|
 |
|
12-26-2005 07:41 PM ET (US)
|
|
Majuzo Kasri ya Mwanazuo (Makene) alitoa wazo: Gazeti Tando. Sijapenda neno gazeti ila neno tando nimelipenda kutokana na ukweli kwamba kwa kutumia blogu zetu hizi tunajenga mtandao ambao unaweza kuona ni kama vile makazi ya buibui yalivyo.
|
| ndesanjo
|
7
|
 |
|
12-26-2005 07:44 PM ET (US)
|
|
Pia Da Mija alipendekeza neno Dimba. Natafuta maana halisi ya neno hili.
|
| Materu
|
8
|
 |
|
12-27-2005 01:00 AM ET (US)
|
|
Napendekeza blog tuipe jina"UWANJA WA FIKRA KOMAVU"
|
| ndesanjo
|
9
|
 |
|
12-27-2005 07:50 AM ET (US)
|
|
Nadhani kati ya maswali ambayo tunapaswa kujiuliza ili tuweze kufanikisha zoezi hili ni hili: je tunachukulia blogu kuwa ni CHOMBO au ni MAHALI?
je blogu ni sehemu unayoitumia kujielezea na kuwasiliana au ni chombo unachotumia kuwasiliana?
|
| ndesanjo
|
10
|
 |
|
12-27-2005 07:52 AM ET (US)
|
|
Nambiza hapo chini kasema jambo moja zuri: neno hili sio vyema likawa refu sana ili liweze kutamkika vyema.
|
| nyembo
|
11
|
 |
|
12-30-2005 06:49 PM ET (US)
|
|
asalam waungwana! mtanisamehe kwa kuwa tabia yangu mara zote ni kuona mambo kinyume zaidi ya fikira za wengine, nimeona Da'Mija umekuwa na wazo zuri sana hapo siendi kinyume nawe, lakini vipi ukatoa msamiati huo "ngwangwa" na zisitumike silabi zingine katika kusaidia herufi "ngw" kwa mfano ngwengwe,ngwingwi,ngwongwo,ngwungwu na kadhalika.
wanazuoni mnaoendelea na mjadala huu mbona hakuna mapendekezo ya majina mnayoyataka nyie kila mmoja anamshauri mwana blog aweke neno badala ya blog huku yeye akiwa hana mchango wowote zaidi ya maneno mengi,oooh mimi nafuatilia kimya kimya nini maana yake, lini ukimya ukazalisha hoja katika jamii ya wanazuoni kama nyie,
lazima tuzungumze na sasa nanena neno langu kwa maana kila mtu anaishi kwa neno alinenalo kwa mujibu wa biblia kwa nini tusitumie neno kama "DURU" KASIRI, LIPULI,VUGA, DONDOO,maneno haya yana maana nzuri katika historia kwa mfano ikulu ya kiongozi wa wahehe katika Tanzania iliitwa LIPULI hili ni baraza la Mzee Mkwawa alipokuwa anapata habari,kufanya maamuzi na kadhalika neno VUGA lina maana kama hiyo kwa Mtemi Kimweri ambae alikuwa mtawala wa maeneo ya Usambaa mwambao wa Pwani ya bahari ya Hindi.
Dondoo ni habari zinazotolewa kwa hali nyembamba walau si katika hali panuzi kama ilivyo kawaida,na Duru hili Sanjari na kuliandika limekuwa neno rahisi masikioni mwetu kwa wale wanaosikiliza idhaa za kiswahili za uingereza na ujerumani hebu litafsirinikwa hakika liende sanjari na neno DIRA,MURUA, na sasa nasema niko Tayari kwa neno lolote lakini litakalo kuwa halina ama haliko mbali na Tafsiri ya matumizi ya neno Blog......
Nimeandika haya hapa juu ili tu iwe ni rahisi kufikisha mawazo yangu kwenu lakini bado nguzo za mjadala huu zibaki kwa Da'Mija na Jeff.....ahsanteni
|
| ndesanjo
|
12
|
 |
|
12-30-2005 06:58 PM ET (US)
|
|
Maneno ambayo yamependekezwa hadi sasa ni: DURU, KASIRI, LIPULI,VUGA, DONDOO, LIPULI, Vuga, UWANJA WA FIKRA KOMAVU, Gazeti Tando, NGWANGA, BAWAZI, na Dimba.
|
| Nyembo
|
13
|
 |
|
12-31-2005 03:40 AM ET (US)
|
|
tehetehe! nashukuru sana Bw, Ndesanjo umenena katika blog yangu kuhusu suala hili la Blog haswa katika la sehemu ama mahali na lile la chombo sasa kuweka sawa hili, walakini bakuli ni chombo lakini ni chombo ambacho ndani yake hutumika kama mahali kwa chakula.
Gari nalo ni chombo lakini ndani yake, hutumika kama mahali pa kusafiria,ama kusafirisha, Blog nayo huenda ni chombo kwa tafsiri yako lakini ndani yake katika (kusherehesha)hii ni lugha ya kiustaadhi sana ikiwa na maana ya kunyambulisha, ni sehemu ni mahali pa kuweka habari,taarifa uchambuzi masomo,vichekesho,na mawazo,mijadala chochote kinacoweza kuandikika,kuchapishwa,nk sioni kama ni vibaya kwa kuangalia upya masuala haya katika mjadala huu kila mjadala na maana halisi ya mwanamjadala huyo anaejadili. ahsanteni
|
| Da Mija
|
14
|
 |
|
12-31-2005 06:46 AM ET (US)
|
|
Nimepeta jina lingine.."PUKUTU".., hili nalo nimelitunga na linaweza kutumika kama ifuatavyo:-
..Tanzania kuna Pukutu nyingi sana. ..Wiki hii nitapukutua juu ya suala zima la afya.
Au nikiichukua ile sentensi ya Ndesanjo isemayo.."Mbona Kasheshe bloguni?"....tunaweza kusema..."Mbona Kasheshe pukutuni?
Halafu washabiki wa Pukutu wataitwa "Wapukutwa"
Bado naendelea kutunga.
|
| Nyembo
|
15
|
 |
|
01-01-2006 06:04 AM ET (US)
|
|
Da Mija nakupongeza sana lakini mimi naona si kazi kutunga tu, tuangalie mnyambuliko wa asili ya neno kwanza Pukutu. kwanza tupange neno tungwa katika kutafuta maana ya ndani ya neno,PAKATA,PEKETE,PIKITI,POKOTO,PUKUTU kisha tunyambulishe kila neno kwa mfano
PAKATA,pakatia,pakatiwa,pakatwa na pakatana,pakatiana pakatika-neno hili lina maana katika kila mnyambuliko wake na maana yenyewe inatumika sana kama kumbatio.
PEKETE,peketia,peketiwa,peketwa,peketana,peketiana,peketika-sioni maana yake katika kiswahili ndani ya mnyambuliko wake kimatumizi.
PIKITI,Pikitia,pikitiwa,pikitwa,pikitana,pikitiana,pikitika- sioni maana yake katika kiswahili ndani ya mnyambuliko wake kimatumizi.
POKOTO,Pokotia,pokotiwa,pokotowa,pokotwa,pokotana,pokotoana,pokotika-sioni maana yake pia ndani ya kiswahili katika matumizi yake.
PUKUTU,pukutia,pukutiwa,pukutuwa,pukutwa,pukutana,pukutuana,pukutika- hapa ndipo ulipo Da Mija, hapa ndipo tulipo waungwana,wanazuoni,watu wa kasrini na barazani.
Na nena kwa kinywa kipana kuwa neno hili katika mnyambuliko wake ukifuatilia hapo juu utakuta kunapatikana matumizi yake katika ulimwengu wa sasa wa lugha ya kiswahili.
Ingawa mwanzoni kunaonekana kama neno Pukutu halina maana halisi walakini kile kinachopukutika kinapukutika katika hali pukutu ama pukutuo, ama pukutuko hapa matunda yanapukutika pukutu pukutu! Katika maeneo yanayotumia kiswahili kama Lamu,Zanzibar,ujiji,Bagamoyo,Tanga,Mombasa,(Nyanza)Burundi huko neno hili linatumika kwa upana mkubwa, si kama napinga bali nachokonoa neno nipate kama linatumika ama halitumiki,isiwe siku moja tukawekwa kitini na kina Said Akida,BW.Mayoka,Profesa Safari na wengineo kulieleza neno hili limetumika vipi hapa ilhali lina zaidi ya maana moja. kama kazi hii ni ngumu zaidi basi tuwape taarifa zaidi Mabaraza ya Kiswahili ya nchi zetu yenye ufafanuzi mzuri wa neno husika BLOG ili mchakato uwe mpana. ahsanteni
|
| Boniphace Makene
|
16
|
 |
|
01-01-2006 12:55 PM ET (US)
|
|
Nilitulia kutazama, nadhani siku ya kutoa maneno imeisha ni kazi ngumu sana hii. Kinachofatia sasa ni wenye maneno kuyapa ushahidi kwa kuangalia nyanja mbalimbali za lugha ya Kiswahili na kuyatetea ili wasomaji wapige kura. Nangoja namri nianze utetezi wa Gzeti Tando.
|
| mark msaki
|
17
|
 |
|
01-02-2006 04:11 AM ET (US)
|
|
jamani mie si mtaalamu sana wa kiswahili. lakini naona hapa tunatumia zaidi top down approach (kutoka juu) kuliko down top (kutoka chini)approach.
ninaunganisha mawazo yaliyotolewa na ninaona hii inampa tabu sana nyembo kwani yeyey7 anauliza ni nini maana ya maneno haya?
maoni yangu ni kwamba labda tuanze na kufafuta zile sentensi zilizopelekea kuanzishwa globu mfano nini nia ya kuanzishwa kwa globu - mfano SEMA USIKIKE inaweza pelekea globu kuitwa payuka/ukelele/ nipashe/ halafu tuzifanyie tafaruki. hapa tutuakutana katikati kwa uzuri kabisa. bila rabsha! - basi kwa sasa labda kaka ndesanjo angetupa kwa muhtasari sentensi inayobeba maana ya globu ili tuifanyie kazi.
kuna maneno mengi yatafanana na ukweli mfano kupembua (kuondoa mawe kwenye mchele )...unaweza kusema naenda kupembua!
au tunaweza kuiita ungo kwani hupepeta kutenga cha kupika na cha kupikwa!
hivi huyu aliyeeiita ngwangwa alikuwa anafikiria nini? kuna embe moja ikiwa changa ni chungu mmno na ikiiva ni tamu sana na ina nyuzi nyingi mithili ya samakai mkonge! sijui alikuwa anafikiria kitu kama hiko?
waheshimiwa wanablogu natoa hoja!
|
| Nyembo
|
18
|
 |
|
01-02-2006 08:23 AM ET (US)
|
|
Mh! sasa Bonny ndio kusema huo ukimya wako ulikuwa unajenga hoja ya kutetea neno lako,sasa naongeza maneno tumiko ambayo yapo katka kiswahili lakini tunahitajika kuyaongezea neno zaidi mbele ili kuleta walau maana halisi ya tukitakacho,"DAFINAPEPE" neno hili lina maana ya (a)Hazina iliyofichwa chini ya ardhi(b)vitu vya thamani vilivyofichwa katika ardhi(c)tunu iliyopatikana bila ya kutarajiwa,nashikilia kifungu cha maana "c" kutumika katika kulihalalisha neno hili DAFINAPEPE, katika blog hizi kunapatikana tunu na vitu ambavyo ni ni kwa njia pepe mnaonaje hata kama ni neno tumiko?
|
| Da Mija
|
19
|
 |
|
01-05-2006 06:04 AM ET (US)
|
|
Kaka Nyembo hebu nisaidie kwanza mwenzio, ..Jina "Mti" lina uhusiano gani na kitu chenyewe kinachowakilishwa? na kama mti ungepewa jina la "mto" na mto ungeitwa "mti" je majina hayo yangeathiri hali ya viwakilishwa hivyo?
Hebu nisaidie kwanza hapo halafu nitajitetea kwa nini napenda kutunga maneno.
|
| ndesanjo
|
20
|
 |
|
01-10-2006 06:43 AM ET (US)
|
|
Da Mija aliwahi kuandika juu ya hili: hakuna uhusiano wowote kati ya jina la kitu na kitu chenyewe. Yaani neno kiti halina uhusiano wa moja kwa moja na kitu tunachokiita kiti. Uhusiano unajengwa na makubaliano na matumizi kwenye jamii. Kingine ni kuwa lugha, maneno, majina huwa yanatungwa na jamii. Na lugha kama ilivyo jamii daima inakuwa na kubadilika. Kunapotokea jambo jipya, maneno ya zamani yanaweza kuvunjwa au kupanguliwa upya ili yakidhi matakwa ya wakati lakini pia ikiwezekana mapya yanaweza kutungwa.
Nakiri kuwa kila siku natafuta suluhisho la jambo hili bila mafanikio. Nadhani maneno pepe na tando yananiingia kidogo kuwa ni sehemu ya neno tutakalochagua. Sisemi tuyatumie kwa wakati mmoja au peke yake ila yakiwepo kama sehemu ya neno zima tutakalochagua. Sababu ni kuwa kati ya jambo linalotofautisha teknolojia hii na teknolojia nyingine za habari kama gazeti, redio, luninga, n.k. ni kwamba hii ni teknolojia pepe. Ni teknolojia ya elektroniki. Inafanyiwa kazi katika mtandao wa tarakilishi. Hivyo kunakuwa na umuhimu fulani wa kipengele hiki muhimu kuwakilishwa katika jina lake. Ni sawa na "email" inavyoitwa baruapepe. Sio barua tu kama tulivyozoea,ile ya kwenda posta. Bali ni barua inayotumia mtandao pepe. Na blogu ndio hivyo. Kwahiyo ninakuwa ninashawishika kiasi fulani kutafuta jina ambalo litaendana na neno "pepe" au "tando."
Asante spika Da Mija, ninaketi.
|
| Da Mija
|
21
|
 |
|
01-10-2006 10:54 AM ET (US)
|
|
Du! Mara nishakuwa mheshimiwa Spika!!!!!!
Asante Mheshimiwa, Je kuna swali la nyongeza juu ya maelezo ya Mheshimiwa Ndesanjo kuhusu uhusiano kati ya jina na kitu kiwakilishwa??
Bungabongo bado inaendelea.
|
| Nyembo
|
22
|
 |
|
01-11-2006 09:07 AM ET (US)
|
|
Assalam mheshimiwa spika Assalam waheshimiwa sana wana mjadala huu Ingawa niliweka baadhi ya maneno yatumike kama maneno mbadala kwa neno blog,lakini nalazimika pia kushawishika na utoaji amri (kama asemayo Da Mija na Ndesanjo "comand" katika kutamka)ili kulitendea kazi neno TANDO na neno PEPE yote kwa pamoja.
Nasema hivi si kwamba naanza kuondoka katika utetezi wa hoja zangu ama kutojibu yote niliyopaswa kujibu kutokana na maswali niliyoulizwa haswa na Da Mija, bali ni huyu Ndesanjo alivyonigusa hapa katika maneno hayo...
Nasema wazi kuwa iwapo tutashurutisha ulimi kutamka maneno haya kama neno moja tu la "TANDOPEPE" ili kupata neno jipya kwa matumizi yetu,basi itakuwa vema kwa kuwa kila kitu kinawezekana.
Kwa nini tuwe na pepe tu au tando tu, hatuhitaji maana wala asili ya neno, tunahitaji amri ya ulimi tu kututhibitishia uwezo wake katika kutamka basi,yatosha kuamrisha sasa neno hilo moja kutoka katika maneno hayo mawili.
Uzuri wa mambo ni kwa uchache,kwa wingi ni maumivu na ghasia, hivyo Mheshimiwa Spika,sasa nawasilisha hoja mpya ya kushurutisha neno Blog liitwe katika Lugha ya Kiswahili TANDOPEPE.
Aidha natoa pongezi kwa wanamjadala walioshiriki na wanaoendelea bila kuchoka,kuunda maneno,kuhakiki,kudadafua,kupinga,kutafsiri,kuyatia ladha nk.
Natumai Hoja hii itaungwa mkono kwa dhati kwa kuwa neno hili licha ya kuonekana jipya kiasi lakini limeundwa toka katika vyanzo pendekezo vya maneno mawili tofauti,pia linaleta maana isiyokimbia uhalisia wa neno linalotafutiwa maana.
nasadiki kuwa neno hilo pendekezo bado linakaribiana na baruapepe,na mengineyo kama alivyotanabaisha Bw. Ndesanjo hapo chini. ahsanteni
|
| Da Mija
|
23
|
 |
|
01-14-2006 09:11 AM ET (US)
|
|
Mheshimiwa Nyembo umeongea. Ninakubaliana na wewe kabisa juu ya jina 'TANDOPEPE', lakini tukumbuke kwamba TANDO si jina jipya lina maana yake tofauti kabisa na masuala ya 'kupashana habari au kupeleka ujumbe' UTANDO/TANDO humaanisha kutandaa au kutapakaa kuliko shikana na ndio maana nyumba ya Buibui inaitwa utando. Leo utakapomwambia mtu BLOG kwa kiswahili ni TANDOPEPE atataka kuhoji kwamba je ukiondoa neno PEPE neno linalobakia yaani TANDO lina maana ileile ya kupashana habari isipokuwa tu habari yenyewe haiko katika kompyuta? Kwa mfano neno BARUA wote tunajua ni njia ya kuandika ujumbe katika karatasi au kitu kinachofanana na hicho, na mtu husoma ujumbe huo katika karatasi au kama ni gome laini la mti linaloweza kuandikika. Lakini neno hilohilo lilipoongezewa neno PEPE ikawa si barua ya karatasi tena bali ya kwenye kompyuta, kwahiyo inakuwa haitatanishi unaposema barua au baruapepe. Ingependeza kama TANDO pekee ingekuwa na maana ileile ya uandishi usio wa kwenye kompyuta. Haya ndio madhara ya kuchagua majina au maneno ambayo tayari yapo yakitumika. Waheshimiwa ninashawishika kuwasilisha tena neno au jina GAZETIPEPE au vinginevyo tulete majina ambayo hayapo kabisa...halafu hivi neno TOVUTI lilitokana na neno gani?
Nawasilisha hoja.
|
| Mwandani
|
24
|
 |
|
01-19-2006 02:33 AM ET (US)
|
|
sasa hapa ndio napapenda. Utaalamu wa lugha na tuendelee kuainisha. Ntakuja na neno langu hivi karibuni Mheshmiwa spika.
|
| Nyembo
|
25
|
 |
|
01-19-2006 02:55 AM ET (US)
|
|
Nashukuru sana! mheshimiwa .Da Mija Shija, Nashukuru pia kwa hoja yako nzito katika wasilisho la gazetipepe, sipati picha kwa neno lililo pendekezo langu kwa nini lisitumike,wakati kuna kanuni ya kushurutisha,kama tunakubaliana na neno Tando kuwa ni kutandaa,na kama Blog ni njia tandao kwa hali pepe kwa nini neno jengwa tandopepe isitumike?
Kwani Blog ni gazeti?nani kasema? vitu vipatikanavyo ndani yake ndio pengine hupatikana gazetini ama katika vyobo vya habari, hii ni njia tandao ya kufikishiana habari,naomba waheshimiwa tusiilazimishe njia hii kuwa gazeti,televisheni,redio ama kipeperushi chochote kwa kuwa tutakuwa tunadanganyana mno!
Aidha waheshimiwa tukumbuke tuliwahi kushindana katika suala la Blog kuwa ni chombo ama mahali?na ninakumbuka mjadala ule uliisha kwa ukavu kwa Mheshimiwa Ndesanjo kuwa kimya ingawa alikuwa kinara mkubwa wa mjadala ule,sasa isiwe kutoka chombo ,mahali, mpaka gazeti.
sina shaka wakati fulani nilifikiri kwa nini neno (Broadcasting)linatumika katika sekta ya habari,"Broad" "cast" ukitoa neno moja lina maana na ukitoa jingine lina maana pia ukiunganisha unapata maana haijalishi kama maana za kila neno hazina uhusiano na neno unganishi jipya! napata ari kuwa neno tando lina maana,neno pepe lina maana na neno jengwa toka katika maneno hayo "tandopepe" litapata maana pia kwa kuwa litahusishwa na kitendo cha husika cha mtandao wa mawasiliano hewa,ambapo ndani yake Ndesanjo huweka umbea,michuzi picha,mkwinda tambo,wewe tenzi,nyembo wowowo nk
nawasilisha hoja mheshimiwa spika kuwa neno hitajiko kwa matumizi mbadala ya neno blog liwe Tandopepe ahsante kwa nafasi hii!
|
| Rama Msangi (Baba Said)
|
26
|
 |
|
01-19-2006 09:51 AM ET (US)
|
|
Kwa heshima ya Mheshimiwa Spika wa Barazapepe, naomba leo niamke usingizini si kwa lengo la kuchangia lolote pengine, ila kwa lengo la kuwaonyesha njia wahjeshimiwa wachangiaji wote.
Kwanza, niwapongeze wote walio, wanao na watakaoshiriki katika mjadala huu hadi kumalizika kwake, maana hawa wameonyesha kumbe tunaweza kabisa kufanya mabadiliko na kuifanya lugha yetu kutoka kuwa ya maneno mengi ya mkopo, na tukawa na yetu wenyewe yakakubalika. Kuna mtu aliwahi kuniuliza kwanini sishiriki, nikamwambia nataka kuona vile mjadala unakuwa kwanza kabla ya kuingia. Naam, na sasa nimepaona kwa hakika.
Nimefurahishwa sana na mameno mbalimbali ambayo washiriki wameyatoa, kuyatetea na kisha kutaka yatumike hayo, ingawa hata hivyo hakuna kati ya hayo ambalo limeweza kukubalika kamili kamili, kuwa sahihi zaidi, na hapa ndipo tunapoona kuwa mapungufu yapo. Kwanini baada ya muda walau kusiwe na neno ambalo walau, hata nusu ya washiriki wanaweza kuwa wanalikubali kuwa linafaa? Tatizo letu ni nini hasa?
Kwa muda wote ambao nimefuatilia mjadala huu, nimebaini kuwa tunapungukiwa kitu kimoja tu, ambacho kuna wakati kilitaka kuzungumzwa lakini kikaachwa njiani sijui kwanini. Tunashindwa kufikia MSINGI wa kile tunachokitafuta. Msingi kwa maana halisi zifuatazo:- Je, BLOGI ni KITU (kifaa, chombo, nk) AU, BLOGI ni MAHALI? (Ukumbi, uwanja, baraza, boma, ukigo, nk)
Nasema hivi kwasababu, asilimia kubwa ya majadiliano ambayo nimekuwa nikiyafuatilia, yanaonyesha kuwa tunachukulia BLOGI kama KITU. Tupo ambao tunaiona ni gazeti labda (gazeti pepe), tupo ambao tunachukulia kama mtandao fulani hivi(TANDOPEPE) na mengi ya aina hiyo. Lakini kweli tuko sahihi?
Kwa mtazamo wangu, Blogi haiwezi kuwa gazeti, kwa maana zile kurasa zetu tunazomili ndio magazeti yenyewe yale -ie- jikomboe.blogspot.com, ni gazetiu pepe linalomilikiwa, kuhaririwa na Bw. Macha nk. Na wala nadhani si sahihi kuliita TANDO PEPE, kwa maana hapa tunakuwa tunazungumzia kitu kama MTANDAO PEPE. Na kama ni hivyo, sisi tunaomiliki blogi, mimi, wewe na yule, tunapoungana ndio tunaunda mtandao - ie- mtandaopepe. Kwa maana sisi makutano, mwingiliano na mawasiliano yetu ni ya ki-elektroniki.
Kwa ujumla, sioni kama inafaa Blogi kuchukuliwa kama kitu, kwasababu, sio kompyuta ambazo tunazitumia, si mashine ya aina yoyote ile ambayo inatumika kutengeneza kitu, bali sehemu ambayo tunahifadhi mawazo yetu, kwa ajili ya wengine kupaona. Kwa hakika, ili kupata urahisi wa kupata neno muafaka hapa, nadhani itakuwa vyema kama tutajadili tukichukulia BLOGI KAMA SEHEMU ya kukutanisha waandishi mbalimbali na wasomaji wao...nk.
Kwanini usiwe UKUMBIPEPE, UWANJAPEPE, DIMBAPEPE, BARAZAPEPE, BOMAPEPE nk? Na wala hatuwezi kuimalizia na kimalizio cha TANDO, kwasababu hapa tunazungumzia juu ya MTANDAO. na kwa mantiki hii kuzema MTANDAO, unakuwa unamaanisha sisi washiriki. Hapa unamaanisha, MTANDAO WA WAANDISHI PEPE, MTANDAO WA WANA-BARAZAPEPE nk.
Bahati Mbaya nimekuja na kasi ile ile ya zamani, ya kusema saaaaaana, hadi kuwachosha. Nashukuru mheshimiwa Spika (Da Mija), na Naomba Kuwasilisha.
|
| Nyembo
|
27
|
 |
|
01-19-2006 10:26 AM ET (US)
|
|
Asante Mheshimiwa spika, kuendelea kuacha nafasi wazi kwa wanaohitaji kuendelea kuchangia mjadala huu na waendelee!
Asante mheshimiwa Msangi kwa mara ya kwanza kusoma mawazo yako, ni muda hasa tumekosa mawazo hapa ya wanamtandao walio wengi na kuambulia wachache ambao pengine wana akili kama za wendawazimu, kwa maana kila kukicha bado wanahangaika kupata muafaka wa mjadala huu kama mwalimu Nyerere na hekaheka za Azimio la Arusha.
Leo nakumbuka mapema niliandika, kuhusu majadiliano yaliyokufa awali bila sababu za msingi haswa sijui Ndesanjo ataweza kulijibu hili maana alikuwa kinara.
Mheshimiwa Msangi amenena kiufaswaha tu, katika mjadala huu, walakini hainisababishi kuondoa neno lile TANDOPEPE bali kulikuza na kulikomaza zaidi ili lipate ruhusa ya kuamriwa kutumika.
sasa nasema hivi! Kama sisi tu wanamtandaopepe wa mtandaopepe kwa nini sehemu,mahala,chomboni ambapo sisi hutandaa ama huwa tunatandaza fikra zetu isiitwe "utandopepe".
Na tukumbuke pia tuliwahi kusema Neno "gazetipepe",mimi ninachosema ni kwamba hewala si utumwa nalikubali neno hili kuwa ni neno pia, lakini vipi neno hili litumike,sitamani kufikiri lakini nalazimika tu kwa kuwa linajadiliwa hapa.
Sidhani kama kuna usahihi wa kuita Blogi, kama gazetipepe, kwasababu, neno gazeti ni kiunganishi tu ambacho kwetu sisi hakina msingi kwakuwa kinachotuunganisha sisi ni kimalizio cha PEPE mwishoni. Tuna vitu kama gazeti la Nipashe, gazeti la Majira, Gazeti la Uhuru, nk, ambayo kwa ujumla wake ndio yanakuwa magazeti. Simaanishi kuwa hatuna magazeti pepe, laa bali kama tukisema magazeti pepe, basi kama alivyotangulia kusema mheshimiwa Msangi, tutakuwa na gazetipepe la Bw. Ndesanjo, gazetipepe la Bw. Msangi, la Da Mija, nk.
Tunachotafuta sisi, sio haya magazeti yetu kuwa tuyaiteje, bali hiki kilichotuwezesha kuanzisha haya magazetipepe, pengine, ndio tukiiteje kwa kiswahili chetu fasaha, na kikakubalika ipasavyo.
Lakini nadhani kwa mtazamo wa mheshimiwa Msangi, kuwa tunatakiwa kujua msingi wa hiki tunachojadili, naamini ni kama tunapata mwanga wa wapi pa kukomalia sote, kuliko kuyumbayumba sana. Tumuunge mkono mheshimiwa Msangi, kuwa tujue msingi wa tunachojadili kwanza kisha tuendelee. Tukubaliane kuwa tunaichukulia kama KITU, KIFAA au ni MAHALI, UKUMBI nk?
Naomba kuwasilisha hoja mheshimiwa Spika wa Barazapepe kwa mujibu pia wa Mheshimiwa Msangi!
|
| ndesanjo
|
28
|
 |
|
01-22-2006 08:10 AM ET (US)
|
|
Ndugu Spika Da Mija, Kwanza kabisa nafurahi kuoana Msangi Mdogo kaingia ukumbini. Tena kwa hoja nzito. Nyembo: uchokozi wangu kuhusu blogu kuwa chombo/kifaa au mahali nilitaka upanuliwe na mjadala wa wengine, na Msangi kafanya hivyo. Kama nilivyosema awali neno "pepe" hadi sasa ndio ninaloafikiana nalo bila pingamizi. Ila maneno yanayokuja nyuma yake bado ninakuwa na mashaka nayo. Kwa mfano, tukisema barazapepe. Tujiulize, blogu na vyumba vya gumzo (chat rooms) zina tofauti gani? Je neno barazapepe linaweza pia kutumika kumaanisha chat rooms?
Tukitazama neno mtandaopepe (toka kwenye tandopepe) tunaweza kujiuliza je tovuti zinaweza kuchukuliwa kuwa nazo zinajenga mtandaopepe? Kama tovuti ni sehemu ya mtandaopepe, je tovuti na blogu ni sawa? Kama sio sawa tofauti ni nini?
Halafu tukisema kuwa blogu ziwe ni gazeti pepe tunaweza kujiuliza je kuna tofauti gani kati ya gazeti lililoko mtandaoni (kama vile Nipashe lililoko kwenye ippmedia.com) na blogu? Je Nipashe unalolisoma mtandaoni ni gazetipepe? Kama jibu ndio, je tunaweza blogu nazo kuziita hivyo? Halafu kuna www.mbongo.com (itembelee) je mbongo.com ni gazetipepe? Kumbuka kuwa tofauti na Nipashe iliyoko mtandaoni ambayo inapatikana pia mtaani, mbongo.com iko mtandaoni tu.
Kwa kufupisha: nini tofauti ya blogu, tovuti, vyumba vya gumzo (chat rooms, magazeti yaliyoko mtandaoni, n.k.? Nadhani ukijiuliza maswali haya na hili linalohusu blogu kuwa mahali au kifaa, utaona kuwa kuna masuala fulani ya kinadharia ambayo lazima tuyatazame kiundani. Kumalizia,Msangi kasema jambo zuri sana: tusipende kutegemea sana lugha za kukopa. Kama sirikali zetu zinapenda kukopa, tusiwe wavivu wa kukopa hata maneno. Nakomea hapa ndugu Spika.
|
| paulkih@yahoo.com
|
29
|
 |
|
01-23-2006 04:03 AM ET (US)
|
|
Ndesanjo Raisi wetu anaitwa Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete.Leo asubuhi nilikuwa Mahakama ya Biashara nikaona picha ya Raisi na hayo maneno.Nikakumbuka Nyerere aliitwa Mwalimu,Mwinyi aliitwa Mtukufu na Mkapa Mheshimiwa!
|
| Boniphace Makene
|
30
|
 |
|
01-23-2006 02:09 PM ET (US)
|
|
Waungwana, kadri siku zinavyokwenda ndipo nenoi "blogu" tulilolitohoa linazidi kukua. Katika Isimu Jamii heshima ya matumizi ya neno hupewa Jamii. Kama jamii inaweza litumia hata hutumie nguvu gani huwezi kubadili. Kuna maneno yaliyowahi pendekezwa na BAKITA yakabakia katika shubaka za kumbukumbu zao. Hayakukubalika kabisa kwa watumiaji. Namna ninavyotazama mjadala huu ukipiga mbio naona mwisho utakuwa neno hili Blogu kubakia maana sasa linaeleweka, linatumika na wengi wameshalitambua.
Kupata jina kwa lugha yetu ni vema lakini si suala la kupendekeza. Kunahitajika utambuzi wa nafasi ya Isimu na maarifa ya uundaji wa maneno katika kila lugha. Huzuni yangu kuwa neno Blogu si letu lakini inatokana na magunduzi haya ambayo hatukuyafanya sisi! Neno "pepe" kumalizika silibaini na sikuwahi kulishabikia na siamini kama lina mhimili sawia katika matumizi na ugunduzi. Nini maana yake. Mtandao kwa maana ya "Website" utaelekea kabisa pale kwenye utando wa buibui unavyojitanua, unavyotandaa. Blogu zinasifa hii pia. Blogu zaweza kuwa sawa na gazeti kabisa huwezi zitofautisha na gazeti la Nipashge lililopo mtandaoni. Blogu yako waweza ichapisha pia na ikapata kurasa kama Nipashe. Ina kila kitu kama hilo gazeti jingine. Maana ya gazeti ni hii ya kupasha na kuandika. Wewe unapasha na kuandika katika blogu lako. Sijui katika mburogu yako ama vingine sijui. Magazeti haya blogu yanasambaa kwa kasi na yana uwezo wa kufikia umati mkubwa kuliko yale ya kuchapishwa kwa karatasi. Hapo ndipo unapopata dhana ya utando, kutanda na kupata kiunganishi anuwai kiitwacho Gazeti Tando.
Nathamini mawazo ya wachangiaji katika kutafuta maana na neno jipya. Lakini wasiwasi wangu ni huu kuwa utafika wakati neno Blogu tunalolitumia na kulitangaza sana katika magazeti ya kawaida katika mwisho wa makala zetu linazoeleka sana. Kumbuka kuna wengi tumefungua Blogu tukizijua tayari kama Blogu na sio vinginevyo. Sasa kuna wengi wanasoma Blogu zetu wakiziita hivyo. Kuna umati mkubwa umekuwa ukimsoma Ndesanjo mwishoni mwa makala zake katika Mwananchi akiweka neno Blogu. Nadhani makala hizo sasa zinatambaa miaka mitatu. Hivyo kupambana na neno lililokaa mitaani kwa miaka mingi hiyo kunahitaji mkakati wa kuangalia wepesi wa wazungumzaji na urahisi wa wao kuelewa na kubakiza dhana tunayoihitaji hapa.
"Gazeti Tando" linabaki neno ninalolibakiza kama pendekezo langu nimekaa muda mrefu kutazama hoja siganifu na zile kinzani lakini hazikunishawishi sana kulitoa neno hili. Nitoe rai pia kuwa wakati wakimbia sana na Blogu linaoota mizizi na mwisho litakuwa na hilo si kosa.
Wasalaam
|
| Kaka Poli
|
31
|
 |
|
01-24-2006 09:37 AM ET (US)
|
|
Habari zenu wote kwa ujumla. Sina mengi ya kudondosha hapa leo, ila ni haya machache sana. Mjadala umeanza kama utani, lakini sasa umekuwa mkubwa na changamoto kadha wa kadha zimetolewa. naunga mkono juhudi zote hizi, ila bado mimi bado nimezembea kidogo katika kufikiria neno blog kwa kibantu wajameni.
|
| michuzi
|
32
|
 |
|
02-22-2006 06:31 AM ET (US)
|
|
asalaam aleikhum wote! najua nimeingia nimechelewa lakini naona hutu twangu tuwili tutatu twaweza changia spidi yetu. awali ya yote mi ningependa neno 'blogu' liendelee na sisi badala ya kuumiza kichwa kwa nini friji lisiitwe kipoza vitu naona tuje na mjadala mpya ambao si mwingine ila kutafuta uongozi rasmi wa wanablogu za kiswahili. yaani kwanza tuunde chama, tukipe jina, kisha tukitafutie nafasi za uongozi na halafu tuchague wa kushika nyadhifa hizo ili mjadala kama huu na ule wa jina la blogu iende kwa mpangilio na si holela, ingawa nia ya blogu ni kuamsha mijadala. ninachotaka kusema ni kwamba mijadala iwe na mwanzo na mwisho. na serikali ama chama ama kamati ama nini sijui itakayoundwa (kama tutakubaliana) iwe ndo neno la mwisho ktk kufunga mjadala aidha kwa kutumia muda ulotumika ama kwa kupiga kura. napendekeza hii iwe serikali ya wanablogu za kiswahili (SWK), na iwe na rais, makamu, waziri mkuu, mawaziri wa wizara zitazopendekezwa na makatibu wakuu na wakurugenzi wa idara husika. kama ilivyo serikali ya tanzania vile, au vipi. wanablogu wote wawe raia. hii ni kutaka kuleta changamoto ambapo wenye wataochaguliwa wawe na majukumu ya kuangalia matukio na mijadala ya wizara zao na kuzileta kwenye kabineti na kufanyiwa mjadala na maamuzi. kwa mfano huu mjadala wa jina ungekuwa chini aidha ya waziri ya habari, utamaduni na michezo na hatimaye rais angeitisha uchaguzi mkuu na kufikia tamati yake.
Naomba nichukue nafasi hii kumpendekeza ndesanjo macha awe rais wa muda, akisaidiwa na mark akiwa makamu wa rais wa muda na damija kama waziri mkuu wa muda. halafu makene awe kaimu spika na jeff msangi awe kaimu spika msaidizi. vyeo vingine vitafuatia endapo itakubalika serikali hii iundwe haraka iwezekanavyo ili tufaidi kublogu. vile vile tungetoa muda na nafasi za watu kutaja nyadhifa muafaka na endapo mtu angependa kushika moja ajitokeze, kampeni zianze na kura zipigwe.
endapo kama serikali ya muda nilopendekeza itakubalika, napendekeza ndesanjo atangaze rasmi kuanzishwa kwa jamhuri ya muungano ya wanablogu za kiswahili, na atangaze baraza lake la muda la mawaziri, ambapo majukumu yake yatakuwa (1) kutunga katiba (2) jina (3) kupanga tarehe ya uchaguzi, kampeni n.k.
naomba kuwasilisha...
|
| Rama Msangi (Baba Saidi)
|
33
|
 |
|
03-01-2006 04:17 AM ET (US)
|
|
Habari za kuumiza vichwa waungwana wa Bunge Pepe. Kwa muda sasa nimekuwa sionekani kuchangia tena katika mjadala huu lakini naamini kabisa kuwa waheshimiwa wote kwa ujumla, wanaendelea vyema katika kuuchangia. Nadhani (japo sina uhakika kama litakuwa wazo lenye kukubalika sana au laa) kuwa kuna umuhimu wa kuelekeza mjadala huu katika kulifanya neno Blogi, kukubalika zaidi kuliko kulibadilisha
|
| Nyembo
|
34
|
 |
|
03-07-2006 08:53 AM ET (US)
|
|
asalamu wajumbe! kuacha kujadili ni udhaifu ulio makini zaidi katika ujuzi wa uchambuzi wa mambo,tena kuacha bila sababu ni ujinga uliotukuka kabisa,ingawa unaweza kuepukika iwapo kila mtu atawajibika,wazo la la Michuzi si baya kabisa ni zuri tu, ila naona tuondoe mfumo wa Serikali na tuweke mfumo wa bunge lenye spika,baraza la mawaziri,wabunge,kiongozi mtetezi wa serikali,na kiongozi wa upinzani bungeni humo,kisha tuwe na vingozi vivuli kwa ajili ya kuwapa changamoto mawaziri husika. uwepo utaratibu wa mzima unaotumika katika bunge la jamhuri yetu hii, na baadhi ya mambo anayo bw. Ramadhani msangi.
|
| ndesanjo
|
35
|
 |
|
03-09-2006 10:43 AM ET (US)
|
|
Michuzi, asante kwa mchango wako na mapendekezo. Naona umependekeza jina langu. Tatizo ni kuwa cheo kama "rais" sikipendi sana. Kama wanablogu wataamua kuunda jumuiya, bunge, jamhuri, serikali, n.k. nitaunga mkono iwapo tutajua kuwa nini madhumuni na malengo yake. Na kama tutahitaji uongozi, nadhani ningependa zaidi kuwa mjumbe (au kama kutakuwa na balozi wa nyumba tano tano au kumi kumi, basi nitagombea huo ubalozi). Tuendelee kujadili.
|
| Da Mija
|
36
|
 |
|
04-17-2006 01:16 PM ET (US)
|
|
Jamani tunasemaje juu ya jina 'GAZETI TANDO' hadi sasa hivi ndiyo limeshika hatamu, Je tunalipitisha? kama tunalipitisha basi tukubaliane kwa pamoja ili tulitangaze rasmi jina hili.
Asanteni.
|
| |
Messages 37-38 deleted by topic administrator between 07-22-2006 02:07 AM and 07-21-2006 09:02 AM |
| Naomi
|
39
|
 |
|
07-21-2006 03:13 PM ET (US)
|
|
Thank You For Creating This Wonderful Resource! Great Work !! Support zyprexa settlement webpage devoted to zyprexa settlement. lasix furosemide webpage devoted to lasix furosemide. too.
|
| |
Messages 40-42 deleted by topic administrator between 07-23-2006 02:08 AM and 08-25-2009 02:06 AM |
| Hamid
|
43
|
 |
|
08-28-2006 04:44 AM ET (US)
|
|
Nakusalimieni kwa njia ya usilam "Usalama na Baraka zake Allah ziwe juu yenu" Nilipenda kuwa nanyi lakini sifahamu lini au suala gani mnazungumzia, naomba anaehusika anijulishe kwa hmdlth@yahoo.com
|
| Luihamu
|
44
|
 |
|
10-29-2006 10:58 PM ET (US)
|
|
Mimi ningependa jina Bloggu litumike kisha Mzee Ndesanjo ateuliwe kuwa rais kama kaka Michuzi alivyopendekeza.Jina Blogu jina muafaka.Jah live.
|
| Mikundu
|
45
|
 |
|
04-21-2007 11:55 AM ET (US)
|
|
|
| Ngurumo
|
46
|
 |
|
07-29-2007 07:25 AM ET (US)
|
|
Edited by author 07-29-2007 07:25 AM
Asante kwa mjadala mzuri. Naona mwelekeo na hitimosho jema. Blogu! Safi sana, na hongera.
www.ngurumo.blogspot.com
|
| Diane
|
47
|
 |
|
09-30-2007 01:58 AM ET (US)
|
|
Alert for all travellers to North America: Racially intolerant white canadian cops and security and their henchmen claim to be despots; following parasitically in the footsteps of their american counterparts, and wilfully engage in their racial profiling of non-whites, in racial harassment of non-whites, and in racially dehumanizing attempts to racially harass non-whites through intimidating physically, mentally, and spiritually; portraying their racial hatred of non-whites through causing wilfull and dehumanizing disturbance to non-whites through using illegal wall-see-through technologies and audio-bugs on non-whites' homes; through listening and watching through the walls of non-whites' rented and owned homes, and through their internet and private telephones. The perpetuators of these evil deeds do this from their cars using illegal equipment slyly given to them by the unworthy cops, and then accelerating their cars loudly and intimidatingly near non-whites' homes and driving intimidatingly in presence of non-whites on streets, making threatening u-turns, driving intimidatingly right up and over sidewalks when a non-white is on the sidewalk, and throwing their ugly bullying weight around, in their shameless acts of cowardice. It is all done slyly, supposedly smartly, however, they cannot fool all the people all the time. The cops also participate themselves to wail their sirens abusively everytime non-whites move and talk inside their rented and owned homes in daily routine living, in addition to having their henchmen in cars commit these ugly harassing racially profiling deeds at all times day and night. Most of these ugly acts of dehumanizing racial profiling depict the cowardice of the doers of these deeds in the real sense, and are done at the behind the scenes insistence of the racially intolerant white cops through their frontline stooges. However, without physical evidence, the white cops, security, socieities, and their henchmen are laughing sinisterly at their heinous deeds and the legal system seems to support this evil through its inability to take action without physical evidence. Their racial profiling penetrates public transport systems, shops and stores to do all they can to make the non-whites feel unwelcome in their dehumanizing acts of racial profiling against non-whites and those who don't conform to their nonsense. The white cops, security, and white communities use their henchmen who do just as they are told and from behind the safety cushion of their oil-guzzling, pollution creating, often dark-glassed vehicles to intimidate and harass non-whites in obnoxious racial profiling that reflects the immoral, despotic, and cowardly behaviour of racially intolerant white cops, security, communities and their dumb henchmen who do just as they are told, fuelled as they are in their racial frenzy, thanks to the racially manipulative corporate controlled media. For more information, visit: http://www.yourluckytoday.blogspot.comVolunteers are welcome to circulate this information to all they know to put an end to this abuse and violations of human rights committed by immorally misbehaved white cops, security, white communities, public transports, shops, stores, etc, and their dumb henchmen who do just as they are told in their racial frenzy.
|
|
|
48
|
 |
|
11-22-2007 07:36 PM ET (US)
|
|
Deleted by topic administrator 02-25-2008 11:12 AM
|
| Heel
|
49
|
 |
|
12-20-2007 03:41 PM ET (US)
|
|
italian news
|
| Dominic
|
50
|
 |
|
12-23-2007 03:08 PM ET (US)
|
|
.
|
kvov0609
|
51
|
 |
|
12-28-2007 09:56 PM ET (US)
|
|
|
| Johno
|
52
|
 |
|
12-31-2007 01:08 AM ET (US)
|
|
|
| saleh/usa
|
53
|
 |
|
01-09-2008 09:23 PM ET (US)
|
|
thank you michuzi for your great news for 20008 keep it up
|
| |
Messages 54-55 deleted by topic administrator between 02-24-2008 08:39 AM and 02-25-2008 11:12 AM |
| Landseer
|
56
|
 |
|
02-03-2008 11:43 PM ET (US)
|
|
|
| quick
|
57
|
 |
|
02-14-2008 01:54 PM ET (US)
|
|
|
| smremont.com
|
58
|
 |
|
02-16-2008 02:08 PM ET (US)
|
|
|
| maria suriano
|
59
|
 |
|
02-17-2008 04:31 PM ET (US)
|
|
---------------------------------
------------------- ------------- L'email della prossima generazione? Puoi averla con la nuova Yahoo! Mail < replied-to message removed by QT >
|
| |
Messages 60-61 deleted by topic administrator 07-25-2009 02:10 AM |
| dsfsdfs
|
62
|
 |
|
02-27-2008 09:28 AM ET (US)
|
|
|
| smremont.com
|
63
|
 |
|
02-27-2008 10:31 AM ET (US)
|
|
|
| smremont.com
|
64
|
 |
|
02-27-2008 10:32 AM ET (US)
|
|
|
| name20
|
65
|
 |
|
02-28-2008 10:27 AM ET (US)
|
|
|
| ssagge
|
66
|
 |
|
03-12-2008 04:37 AM ET (US)
|
|
|
| Denis
|
67
|
 |
|
04-06-2008 02:57 PM ET (US)
|
|
|
| den
|
68
|
 |
|
04-17-2008 12:23 PM ET (US)
|
|
|
| |
Messages 69-72 deleted by topic administrator between 05-17-2008 10:14 AM and 05-15-2008 02:43 AM |
| 瑙韲瑪褪韈
|
73
|
 |
|
06-13-2008 04:45 PM ET (US)
|
|
|
| |
Messages 74-75 deleted by topic administrator between 07-03-2008 02:45 AM and 10-07-2008 02:29 AM |
| 43214312
|
76
|
 |
|
07-03-2008 11:21 PM ET (US)
|
|
1431243214
|
| |
Messages 77-87 deleted by topic administrator between 07-10-2008 02:41 AM and 10-06-2008 02:25 AM |
babysmiling
|
88
|
 |
|
07-11-2008 12:13 AM ET (US)
|
|
Need to know before buying Lace wigs
|
| dmtr
|
89
|
 |
|
07-21-2008 05:11 AM ET (US)
|
|
|
| dmtr
|
90
|
 |
|
07-21-2008 05:20 AM ET (US)
|
|
|
| Dima
|
91
|
 |
|
07-21-2008 05:21 AM ET (US)
|
|
|
| Dima
|
92
|
 |
|
07-21-2008 05:22 AM ET (US)
|
|
|
| Dima
|
93
|
 |
|
07-21-2008 05:22 AM ET (US)
|
|
|
| |
Messages 94-104 deleted by topic administrator between 10-07-2008 02:29 AM and 07-22-2008 05:12 AM |
| Jennifer
|
105
|
 |
|
09-06-2008 06:26 AM ET (US)
|
|
As Chairman of The Winnick Family Foundation, Gary Winnick gives a great deal of time and energy to philanthropic causes. In addition to supporting wonderful initiatives such as the state- of-the-art clinical research at Cedars-Sinai Medical Center
|
| |
Messages 106-115 deleted by topic administrator between 09-17-2008 08:45 AM and 10-07-2008 02:29 AM |
| ppsxhuyhsf
|
116
|
 |
|
09-18-2008 10:12 AM ET (US)
|
|
|
| |
Messages 117-118 deleted by topic administrator 10-07-2008 02:29 AM |
| warhammer
|
119
|
 |
|
09-26-2008 04:55 AM ET (US)
|
|
|
| |
Messages 120-134 deleted by topic administrator 10-07-2008 02:29 AM |
| wow gold
|
135
|
 |
|
11-29-2008 12:03 AM ET (US)
|
|
|
| wow gold
|
136
|
 |
|
11-29-2008 12:38 AM ET (US)
|
|
garmhellhammer@gmail.com
|
ericbin1
|
137
|
 |
|
12-24-2008 10:26 PM ET (US)
|
|
|
| wow gold
|
138
|
 |
|
02-15-2009 09:25 PM ET (US)
|
|
Want to save huge expenditure will be able to buy more wow gold ? As soon as possible to mmoinn.com! We provide you with more and better cheap wow gold and wow power leveling . Here is a professional trade platform, you will get a guarantee of confidence!
|
| wow gold
|
139
|
 |
|
03-15-2009 02:53 AM ET (US)
|
|
|
|
|
140
|
 |
|
04-15-2009 01:30 AM ET (US)
|
|
Deleted by topic administrator 07-25-2009 02:10 AM
|
| blueangle
|
141
|
 |
|
06-12-2009 03:21 AM ET (US)
|
|
|
| Aimersoft DVD Creator
|
142
|
 |
|
06-12-2009 06:53 AM ET (US)
|
|
If you need convert your video to DVD, Aimersoft dvd creator is a good choice. It's professional software to convert and burn video to DVD (also can convert and burn iTunes videos/YouTube FLV movies/ AVI files/QuickTime movies/MKV Files etc. to DVD). It's powerful and easy-to-use to convert and burn your favorite videos to your computer or your blank DVD Disc as backup. It's with high compatibility and great quality. With this DVD backup software, you will never need to worry about backup your DVD.
|
| Nsanvlrc
|
143
|
 |
|
06-25-2009 01:12 AM ET (US)
|
|
dUIbOM comment5 ,
|
| extract mp3 from youtube
|
144
|
 |
|
07-01-2009 02:10 AM ET (US)
|
|
How to extract mp3 from YouTube videos, FLV videos? YouTube is by now the most popular online music provider, if you want to extract mp3 from YouTube Videos, they will plug-in a video converter, which can convert YouTube flv to mp3. Generally, it may lose lots of quality while converting video to audio mp3. Wondershare Streaming Audio Recordera streaming mp3 recorder to extract mp3 from YouTube, extract mp3 from flv with high quality. http://www.download-streaming-video.com/st...lv-youtube.html#159
|
| jack
|
145
|
 |
|
07-06-2009 11:33 PM ET (US)
|
|
Wondershare Streaming Audio Recorder is a professional tool to download, record aol radio music to mp3, WMA, AAC, AC3 etc.
|
| replica rolex
|
146
|
 |
|
07-14-2009 04:59 AM ET (US)
|
|
The replica rolex Date is 34mm like the Air-King, but it obviously includes a date function. IIts production began in the late 1950s around the time the steel Datejust was introduced. Retails range from $5,250 with a smooth bezel and Oyster bracelet to $7,000 with an 18K white gold fluted bezel and diamond markers, to $15,050 for 18K Yellow gold on a jubilee bracelet. rolex replica model was once offered in 3 flavors: steel, 18k yellow & steel, and all 18k yellow gold. replica rolex watches ares now only available in steel or solid yellow gold and replica watches
|
| Eosfbxad
|
147
|
 |
|
07-14-2009 07:34 AM ET (US)
|
|
U3dC29
|
| Ylaupjok
|
148
|
 |
|
07-14-2009 08:17 AM ET (US)
|
|
GY9whY
|
|
|
149
|
 |
|
07-14-2009 11:36 PM ET (US)
|
|
Deleted by topic administrator 07-16-2009 02:06 AM
|
| Bkwrpmxg
|
150
|
 |
|
07-15-2009 08:33 AM ET (US)
|
|
HYmlhh
|
| Uqrhezpn
|
151
|
 |
|
07-15-2009 02:28 PM ET (US)
|
|
N6EiT2
|
| Shkroszg
|
152
|
 |
|
07-15-2009 06:16 PM ET (US)
|
|
p4DS3t
|
|
153
|
 |
|
07-21-2009 10:46 PM ET (US)
|
|
Deleted by topic administrator 08-25-2009 02:06 AM
|
| download imeem songs
|
154
|
 |
|
07-22-2009 10:39 PM ET (US)
|
|
With "setting","record" and "browse" just 3 steps, you will be free to download imeem music and then save imeem songs. Don't be just waiting, try Audio Recorder now. Sure you will like the stuff to download imeem songs and save imeem songs, enjoy them freely.
|
|
|
155
|
 |
|
07-23-2009 05:06 AM ET (US)
|
|
Deleted by topic administrator 08-25-2009 02:06 AM
|
| beverly ma restaurant som
|
156
|
 |
|
07-25-2009 05:50 AM ET (US)
|
|
If you have to do it, you might as well do it right.
|
| Streaming Video Recorder
|
157
|
 |
|
07-28-2009 10:32 PM ET (US)
|
|
How to download MySpace music? Have you ever thought about extract MP3 from FLV? Thats easy, Wondershare Streaming Audio Recorder is the best tool which has been proved by many users to download MySpace music and extract MP3 from FLV. Meanwhile, want to download Google Video? Streaming Video Recorder is your best choice. YouTube Downloader is a professional one to let you download YouTube videos freely. Believe it or not, these software will surprise you a lot.
|
| rip music from YouTube
|
158
|
 |
|
08-24-2009 02:15 AM ET (US)
|
|
Edited by author 08-24-2009 02:16 AM
Many times there is a cool music on YouTube or similar sites. You just need to have it but cannot find how. Actually, there are several ways to rip YouTube music, but I think that using the YouTube music ripper - Streaming Audio Recorder is the best way. This software is designed to record any streaming audio from internet radio stations and web-based audio sources. Using Streaming Audio Recorder, you can simply rip music from YouTube and save to your PC.
|
| fake rolex watches
|
159
|
 |
|
09-22-2009 02:23 AM ET (US)
|
|
|
| dvd creator
|
160
|
 |
|
09-27-2009 06:15 AM ET (US)
|
|
|
| badboy
|
161
|
 |
|
10-16-2009 02:31 AM ET (US)
|
|
Edited by author 10-16-2009 02:35 AM
How to burn video to dvd,where to find the best dvd creator.Here i introduce a dvd creator,it's a powerful video DVD maker which helps you easily convert all videos to DVD including AVI, MPG, MPEG, MP4, WMV, MOV, MP4, DAT, RM, and HD videos such as M2TS, TP, TRP, etc. You can even make a video slideshow with 32 menu templates and 60 transition effects.
|
| progiftstore
|
162
|
 |
|
10-28-2009 04:39 AM ET (US)
|
|
|